Posts

Showing posts from March, 2021

EYMAEL: KUIFUNGA SIMBA MBELE YA JPM NI KUMBUKUMBU KWANGU NA WACHEZAJI

Image
   LUC Eymael, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2019/20 amesema kuwa moja ya kitu ambacho anakikumbuka muda wote ni ushindi wake mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 8,2020 na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Simba. Bao pekee ambalo alilishuhudia pia aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli lilipachikwa kimiani na Bernard Morrison na kuwafanya Simba wayeyushe pointi tatu. Kwa sasa baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki Machi 17,2021 Samia Suluhu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa katiba ambapo awali alikuwa ni makamu wa JPM. Leo Machi 30, Samia amemchagua Philip Mpango awe Makamu wa Rais wa Tanzania ambapo jina lake limepitishwa na Wabunge kwa asilimia 100. Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael ambaye kwa sasa yupo Ubelgiji amesema kuwa anakumbuka mchezo huo kwa namna ambavyo Magufuli aliweza kuhudhuria na timu yake ilishinda jambo ambalo hal...

AS VITA WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA WAANZA KUMWAGA SABABU KIBAO

Image
    ZIKIWA zimesalia siku chache kufikia siku ya mtanange kati ya Simba na AS Vita, Kocha Mkuu wa AS Vita kutoka nchini DR Congo, Florent Ibenge ameweka wazi kuwa ratiba yake ya sasa si rafiki kwa klabu hiyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba. Ibenge ukiachana na kuwa kocha wa AS Vita, pia ni kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Congo ambapo Jumatatu aliongoza taifa la Congo katika mchezo wao wa mwisho wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika dhidi ya Gambia. Kwenye mchezo huo Ibenge alishuhudia kikosi chake kikishinda bao 1-0 ila kilikwama kufuzu Afcon nchini Cameroon kwa kuwa kipo nafasi ya tatu.   Ibenge amesema kuwa ratiba ya mechi za timu za taifa na michuano ya Ligi ya Mabingwa imebana sana kiasi cha kukosa siku za kutosha kwake kukiandaa kikosi cha AS Vita kuelekea mchezo wao unaofuata wa michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Simba.     “Ratiba si rafiki kwetu, nadhani hii ni kwa klabu nyingi zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa, ukiangalia mechi za timu za...

KOCHA BIASHARA UNITED KUANZA KUONGEZA MAKALI YA WASHAMBULIAJI

Image
   KOCHA Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Francis Baraza amesema kuwa kazi ya kwanza atakayoanza nayo kwa sasa ni kushughulika na safu ya ushambuliaji ili irejeshe makali yake. Baraza amechukua mikoba ya Mecky Maxime ambaye alifutwa kazi kutokana na mwendo mbovu wa timu yake na mchezo wa mwisho kukaa benchi ilikuwa mbele ya Azam FC ambapo ubao wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 1-2 Azam FC. Kwa sasa Maxime yupo huru ambapo amekuwa akitajwa kuibukia Biashara United kuchukua mikoba ya Baraza. Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa amewatazama washambuliaji wake walivyo na ameona ni lazima aanze nao ili kuongeza kasi kwenye ushambuliaji. "Ili timu ipate ushindi ni lazima ifunge na ufungaji unaanzia kwa washambuliaji pamoja na viungo ambao kazi yao ni kutengeneza nafasi za kufunga kwa washambuliaji. "Kikubwa ambacho nina amini kwamba kinawezekana ni kupata matokeo katika mechi zetu hivyo mashabiki watupe sapoti bila kuwa na mashaka nasi," . Kagera Sugar kwenye msimamo ipo...

BODI YA LIGI YATAJA SIKU YA MECHI ZA LIGI KUU BARA PAMOJA NA KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA

Image
  ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea Aprili 8 baada ya kutimiza siku 21 za maombolezo. Ligi ilisimama kwa muda kutokana na msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Joseph Magufuli ambapo zilitolewa siku 21 za maombolezo. Magufuli alitangulia mbele za haki Machi 17 jambo lilipolekea Serikali kutoa siku 21 za maombolezo ambazo bado zinaendelea kwa sasa. Kasongo amesema:- "Ukitazama ratiba yetu ile ya awali ambayo tuliitoa kwa vilabu ilikuwa inaonyesha kwamba tarehe 3-4 Machi, michezo ya Kombe la Shirikisho, tarehe 6-8 Machi tulikuwa tunarejea kwenye mechi za ligi. "Kutokana na msiba tafsiri yake ni kwamba ile michezo ya Shirikisho na ile ya ligi nayo inakuwa haipo kwa sababu tupo kwenye maombolezo ya siku 21. "Kumbuka kwamba siku 21 zinaisha tarehe 7 ambapo kulikuwa na mchezo wa ligi, tarehe 6 kulikuwa na mchezo wa ligi na tarehe 3-4 kulikuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho. ...

SIMBA HATA HAWAJUI ALIPO MSHAMBULIAJI WAO LOKOSA

Image
  KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Didier Gomes amesema kuwa hajui alipo mshambuliaji wake Lokosa Junior. Junior raia wa Nigeria alisajiliwa na Simba kwa dili la miezi 6 na sababu kubwa ya usajili wake ni kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Akiwa ndani ya kikosi cha Simba hajaweza kuonekana kwenye mechi ya ushindani ambapo Simba ikiwa imecheza mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi hajacheza mchezo hata mmoja. Nafasi yake ya ushambuliaji amekuwa akianza Chris Mugalu pamoja na Meddie Kagere ambaye mechi nyingi amekuwa akianzia benchi huku John Bocco taratibu akirejea kwenye ubora wake. Katika mazoezi ya Simba ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Simba Mo Arena vilivyoppo Bunju, Lokosa hajaonekana mazoezini huku habari zikieleza kuwa amevunjiwa mkataba wake na mabosi hao wa mtaa wa Msimbazi. Kuhusu Lokosa, Gomes amesema:"Sijui kwa kweli kuhusu huyo, ila siwezi kulizungumzia jambo hilo ila ukweli ni kwamba sijamuona muda mrefu kwenye eneo la mazoezi,...

VURUGU ZA LIGI KUU BARA NI MPAKA JULAI BADALA YA KUISHA JUNI

Image
   ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) amesema kuwa msimu wa 2020/21 utakamilika Julai tofauti na awali ambapo ulitarajiwa kukamilika Juni. Mabadiliko hayo ya muda wa ligi kukamilika yametokana na kutokea kwa msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli ambaye alitangulia mbele za haki Machi 17. Kutokana na msiba huo ambao ni mkubwa kwa Tanzania na Afrika kiujumla kulikuwa na siku 21 za maombolze ambazo zinaendelea mpaka wakati huu na zinatarajiwa kukamilika Aprili 7. Kasongo amesema:" Awali ligi yetu ya Tanzania Bara ilipaswa kumalizika tarehe 12 mwezi wa sita lakini kulingana na mabadiliko ligi itaisha tarehe 11 mwezi wa saba. "Hii inatokana na kuwa na mabadiliko ambayo yamefanyika kwenye ligi kuendena na siku 21 ambazo ni za maombolezo," . Leo TBLB imetoa ratiba ambayo inaonyesha kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mechi za Kombe la Shirikisho zitarejea kuanzia Aprili 8. Kwa timu ambazo zitaangukia kucheza Playoff 2020/21...

KOCHA MPYA YANGA ATOA NENO LA MATUMAINI

Image
  BAADA ya kupewa dili la miezi mitatu kuinoa Klabu ya yanga, kocha mpya wa makipa  Razak Siwa amesema kuwa anaamini atafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Kocha huyo raia wa Kenya alitambulishwa rasmi jana, Machi 29 na tayari ameanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kinachosimamiwa na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi. Mwambusi amechukua mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7,2021 kutokana na matokeo mabovu kwa mujibu wa mabosi wa Yanga ambapo mzunguko wa pili kwenye mechi 6 alishinda moja na kuambulia kichapo moja huku nne akiambulia sare. Nizar Khalfan ambaye alikuwa msaidizi wake naye alifutwa kazi huku kocha wa makipa Niyonkuru raia wa Burundi naye akichimbishwa na nafasi yake imechukuliwa na Siwa. Siwa amesema:"Nimefurahi kuwa hapa na nitatoa ushirikiano mkubwa na kila mchezaji pamoja na uongozi kiujumla," .

AS VITA: YAPIGA HESABU KUIFUNGA SIMBA KWA MKAPA

Image
  FLORENT Ibenge, Kocha Mkuu wa AS Vita amesema kuwa watapambana kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao dhidi ya Simba ili waweze kutimiza malengo ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. AS Vita inakumbuka kwamba ilipokutana na Simba mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba. Bao lililowapa Simba pointi tatu lilifungwa na Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti na kuwafanya wasepe ugenini wakiwa kifua mbele. Kwenye msimamo wa kundi A, AS Vita ina pointi nne huku Simba ikiwa na pointi 10 inaongoza kundi inafuatiwa na Al Ahly nafasi ya pili yenye pointi 7. Imekuwa ikipata matokeo ugenini AS Vita kwa kuwa pointi zote nne ilikusanya ugenini ilishinda mbele ya Al Merrikh inayoshika nafasi ya nne na pointi moja na ililazimisha sare mbele ya Al Ahly. Ibenge amesema:"Tunahitaji kushinda mchezo wetu ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu uhitaji wetu ni kuona kwamba tunaweza kutinga hatua ya robo fainali. "Wapinzani wetu Simba ...

RATIBA YA SIMBA APRILI NI MOTO, CHEKI VIGONGO VILIVYO

Image
  DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba ana kazi ya kufanya ndani ya Aprili kukiongoza kikosi chake kusaka pointi tatu kwenye mechi zake 6 ambazo ni dakika 540 za moto. Mechi hizo ni dhidi ya AS Vita Club Aprili 3, mchezo wa kwanza walipokutana nchini DR Congo, ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba, Al Ahly ya Misri Aprili 9, mchezo wa kwanza ubao ulisoma Simba 1-0 Al Ahly, hizi mbili ni dakika 180 za kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa upande wa Ligi Kuu Bara atakuwa na kazi mbele ya Kagera Sugar, Aprili 14, Uwanja wa Kaitaba na mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja Wa Uhuru ubao ulisoma Simba 2-0 Kagera Sugar. Pia ana kazi mbele ya Dodoma Jiji ni Aprili 18, mchezo wa kwanza Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Simba ilishinda mabao 2-1, Coastal Union ni Aprili 25 mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Simba ilishinda kwa mabao 7-0.  Funga kazi kwa Gomes itakuwa ni Aprili 28 dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Simba ilipokutana kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Jamhuri, Moro...

AS VITA : TUNAIFUNGA SIMBA TUKIJA TANZANIA

Image
  M SHAMBULIAJI wa  AS Vita, Ducapel  Moloko, amewapiga  mkwara mzito  Simba kwa kusema  kuwa watachukua alama tatu  watakapokutana uwanjani  Jumamosi hii.   Kauli hiyo ameitoa zikiwa zimebaki  siku chache kabla timu hizo  hazijavaana kwenye mechi ya hatua  ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika  itakayochezwa wikiendi hii kwenye  Uwanja wa Mkapa, Dar.  Moloko amesema kuwa,  wamejipanga kuchukua ushindi kwa  Simba ili kutengeneza nafasi ya kufuzu  hatua ya makundi. “Sisi tumejiandaa na tutaifunga  Simba ikiwa nyumbani kwao na alama  zote tutazichukua, subiri tuje mtauona  moto wetu,” alisema mshambuliaji  huyo.   Katika michuano hiyo, Simba ndiyo  vinara wa Kundi A wakiwa na pointi  10, wakifuatiwa na Al Ahly yenye  saba, huku AS Vita ikijikusanyia pointi  nne na Al Merrikh moja.  Timu zote  zimecheza mechi nne zikibakiwa na  mbili kukamili...

MORRISON APEWA UJUMBE WA KUFANYIA KAZI NA MFARANSA WA SIMBA

Image
  KOCHA Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema kuwa kiungo wake mshambuliaji Bernard Morrison ana uwezo mkubwa ila anapaswa aongeze umakini zaidi akiwa uwanjani. Gomes, raia wa Ufaransa amesema kuwa amekuwa akifurahishwa na wachezaji wake wote wakiwa kwenye majukumu yao ila wakati mwingine Morrison amekuwa ni mtu mwenye utani mwingi. Morrison alikuwa sehemu ya kikosi kilichowavaa Al Merrikh Uwanja wa Mkapa wakati wakishinda mabao 3-0 na kuwafanya wasepe na pointi tatu huku yeye akitengeneza pasi moja ya bao kwa Mohamed Hussein. Kiungo huyo alikuwa kwenye ubora wake na alionekana kuwa na maamuzi ya haraka jambo lililomfurahisha Gomes. Kuhusu uwezo wa mchezaji huyo Gomes amesema:"Morrison ni mchezaji mzuri ila kuna wakati mwingine amekuwa ni mtu wa utani, sasa ikiwa timu inahitaji ushindi ni lazima utani uwekwe kando kisha kazi ifanyike. "Kila mchezaji ndani ya Simba ana uwezo wake na wanategemeana katika kusaka ushindi, bado safari ni ndefu kwani tunahitaji pointi moja ili kufikia...

MICHAEL SARPONG ANAPENDA KUFUNGA

Image
  MICHAEL Sarpong, mshambuliaji wa Klabu ya Yanga amesema kuwa kitu ambacho anakipenda kukifanya akiwa uwanjani ni kufunga mabao kwa ajili ya timu yake. Nyota huyo raia wa Ghana ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga kilicho chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi aliyechukua mikoba ya Cedric Kaze aliyefutwa kazi Machi 7. Aliibuka Yanga akitokea Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda na kusaini dili la miaka miwili kuwatumikia Wanajangwani. Yanga ikiwa imetupia jumla ya mabao 36  kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 23 amehusika katika mabao matano ambapo amefunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao. Sarpong amesema:-"Nikiwa uwanjani ninapenda kufunga na kuipa ushindi timu yangu hakuna jambo jingine ambalo huwa ninapenda. Ikitokea nikashindwa basi nitatengeneza nafasi kwa mwenzangu. "Ukweli ni kwamba mashabiki wanapenda kuona timu ikishinda hilo ninalijua hata mwalimu pia amekuwa akituambia suala hilo, imani yangu nitafanya hivyo katika mechi zetu zijazo," . Sarpon...

MFARANSA WA SIMBA AFICHUA KINACHOWABEBA KIMATAIFA

Image
  DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kikubwa ambacho kinawapa nguvu ya kuamini kwamba watapata matokeo mbele ya AS Vita ni pamoja na hali ya kujiamini na maandalizi mazuri. Kikosi cha Simba kinatarajiwa kumenyana na AS Vita kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.   Mfaransa huyo ameongeza kwamba kuchukulia siriazi na kujiamini katika mechi zao ndiyo kitu ambacho kimekuwa kikiwabeba na kuifanya timu hiyo kutopoteza mechi yoyote hadi sasa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.   Simba ni vinara wa Kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika watakuwa uwanjani kupambana na Vita katika mechi ambayo Simba wakitoa sare tu watajihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali, lakini Vita wanahitaji ushindi tu ili wafufue matumaini yao ya kutinga robo fainali.    Gomes  amesema kwamba kila mechi ambayo wamekuwa wakiicheza katika hatua hiyo wamekuwa wakiamini kwamba wanaweza kupata matokeo na hiyo imekuwa msaada mkubwa...

MSHAMBULIAJI MPYA SIMBA LOKOSA AVUNJIWA MKATABA, ATOWEKA

Image
    UONGOZI wa Simba, umelazimika kuachana na mshambuliaji wao raia wa Nigeria, Lokosa Junior, baada ya kutoweka kwa siku tatu kwenye mazoezi ya timu hiyo.   Lokosa alijiunga na Simba miezi miwili iliyopita akitokea timu ya Esperance ya Tunisia, aliyokuwa akiitumikia kabla ya kurejea kwao Nigeria ambapo alikuwa nje ya dimba kwa zaidi ya miezi nane.   Simba walimsajili mshambuliaji huyo wakiamini angeweza kurejea kwenye kiwango chake na kuwasaidia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.   Chanzo chetu kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Championi Jumatano kuwa, tayari mabosi wa Simba wamevunja mkataba kimyakimya na nyota huyo, jambo lililomfanya ajiondoe rasmi kwenye mazoezi ya timu hiyo akisubiria maslahi yake ya kuvunjwa kwa mkataba huo ili arejee kwao kujipanga na timu nyingine. “Nimeamini kweli kwenye mpira mchezaji kama akikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, rekodi yake pekee haiwezi kumlinda, maana juzi nilimsikia mazoezini kocha wetu, Gom...

LUIS:KUONDOKA KWA MAGUFULI HASARA KWA AFRIKA

Image
  KUTOKANA na kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kilichotangwazwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Machi 17, kiungo wa Simba Luis Miquissone amesema kuwa ni hasara kwa Arika na Dunia kiujumla. Kiungo huyo raia wa Msumbuji amesema kuwa ni wakati mgumu ambao Watanzania wanapitia kwa sasa.  Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Hasara kubwa kwa watu wa Tanzania, Afrika na ulimwengu wote. Mungu aipe familia na watu wa Tanzania nguvu wakati huu mgumu," ,

ZIMBWE JR AWEKA REKODI YAKE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
  MOHAMED Hussein, ’Zimbwe’  nahodha msaidizi wa Klabu ya Simba bao lake mbele ya Al Merrikh limeweka rekodi Afrika kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga katika hatua ya makundi ndani ya kikosi hicho. Chini ya Didier Gomes, Simba inayoongoza kundi A na pointi 10, imefunga jumla ya mabao matano manne yote yalifungwa na wageni hivyo bao lake limeweka rekodi kwa msimu wa 2020/21. Mabao hayo ya Simba yalifungwa na Chris Mugalu mwenye mabao mawili, mbele ya AS Vita na Al Merrikh yeye ni raia wa Congo, Luis Miquissone ana mabao mawili alifunga mbele ya Al Ahly na Al Merrikh. Bao la kwanza la mzawa ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Simba limefungwa na Zimbwe, Uwanja wa Mkapa yeye ni beki wa kushoto chaguo namba moja la Gomes.  Pia jina limetajwa kwenye orodha ya kikosi bora cha wiki ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi nne hivyo anakuwa mzawa wa kwanza kuingia kwenye kikosi.

MSUVA AITAMANI SIMBA ROBO FAINALI CAF

Image
  WINGA wa klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morroco, Saimon Msuva amesema kuwa anatamani kukutana    na klabu ya Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani anaamini itakuwa mechi nzuri sana katika msimu huu wa ligi hiyo. Saimon Msuva katika msimu huu wa ligi hiyo akiwa na klabu ya Wydad Casablanca ya Morroco amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao miwili katika michezo minne aliyocheza mpaka sasa. Akizungumzia michuano hiyo Msuva amesema:  “Natamani kuona tunakutana na Simba katika hatua ya robo fainali kwani utakuwa mchezo mzuri sana katika ligi ya mabingwa msimu huu kwani itazikutanisha timu bora ambazo zote zinafanya vizuri kwa sasa.

MASTAA SITA SIMBA WAIFUNIKA YANGA

Image
  “WAMEFUNIKA” ndivyo unavyoweza kusema, kwani unaambiwa mastaa sita tu wa kikosi cha Simba wamefanikiwa kufunga mabao 36, ambayo ni idadi sawa na mabao yote yaliyofungwa na nyota wa kikosi cha klabu ya Yanga. Mastaa hao sita wa Simba ni Meddie Kagere, John Bocco, Clatous Chama, Bernard Morrison, Chris Mugalu na Luis Miquissone. Katika mchanganuo huo Kagere amefunga mabao 9 sawa na John Bocco, Clatous Chama 6, Chris Mugalu 5, Miquissone 4 na Morrison 3. Simba ndiyo timu ambayo imefunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa na mabao 46 huku yanga wao wakiwa katika nafasi ya pili na mabao 36. Simba pia ndiyo timu iliyofungwa mabao machache zaidi kwenye ligi, mabao 9 ikifuatiwa na Yanga waliofungwa mabao 14.

AS VITA, TP MAZEMBE WAMLILIA RAIS MAGUFULI

Image
  BAADA ya kusikia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania John Magufuli, kiungo wa kati wa Klabu ya AS Vita, Jeremy Mumbere amemlilia rais huyo huku akisema kuwa yeye alikuwa ni kati ya shabiki mkubwa wa kiongozi huyo.     Jeremy Mumbere kwa sasa ni nahodha wa kikosi cha AS Vita na timu ya Taifa ya DR Congo.   Akizungumza na Championi Ijumaa moja kwa moja kutoka nchini DR Congo, Mumbere alisema kuwa amesikitishwa kusikia taarifa za kifo cha Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kwani alikuwa ni kiongozi mzuri ambaye alikuwa akimfuatilia kwa ukaribu kutokana na utendaji wake kuwa mzuri jambo ambalo lilimfanya awe anamfuatilia mara kwa mara.   “Nimesikitika sana kusikia taarifa za msiba wa Rais wa Tanzania, John Magufuli ni moja kati ya rais bora kuwahi kutokea katika bara hili la Afrika, alikuwa ni kiongozi anayependa maendeleo na Tanzania ilikuwa imepata mengi mazuri kutoka kwake.   “Utendaji wake wa kazi ulinifanya niwe shabiki yake kwa kumfuatilia kwa mambo men...

YANGA YASHUSHA PRESHA MASHABIKI WAKE, KUREJEA KWENYE UBORA

Image
    UONGOZI wa Yanga umewaomba mashabiki wasiwe na presha juu ya mwendo wao ndani ya ligi kwa kuwa wanaamini kwamba watarejea kwenye ubora. Machi 7, Yanga walimfuta kazi Cedric Kaze raia wa Burundi na msaidizi wake Nizar Khalfan ambaye ni mzawa kwa kile ambacho walieleza kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo. Kwenye mzunguko wa pili kwenye mechi sita, Kaze aliongoza kikosi hicho kushinda mechi moja, sare nne na alipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union. Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa yote ambayo wanapita ni kipindi cha mpito yatakwisha na maisha yataendelea. “Tukiwa ni timu tunatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona tunapata matokeo hilo ni jambo jema nasi tunalifikiria. Kuyumba ni kwa muda tunaamini kwamba tutarejea kwenye ubora na kila kitu kitakwenda sawa. “Ikiwa shabiki utasema ukate tamaa wakati huu bado ni mapema na ligi haijakamilika, hivyo muhimu ni kubaki kwenye malengo yetu na kuzidi kupambana,” .

SIMBA YAPANIA KUTIMIZA AHADI YA MAGUFULI KWA VITENDO

Image
    UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utapambana kutimiza agizo la Rais wa awamu ya tano, John Magufuli la kuwataka watwae ubingwa wa Afrika. Agizo hilo alilitoa msimu wa 201//18 wakati akiwakabidhi ubingwa wa Ligi Kuu Bara na alishuhudia timu hiyo ikitunguliwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar. Magufuli ambaye alitangazwa kufikwa na umauti Machi 17 na Makamu wa Rais, Samia Suluhu ambaye kwa sasa ni Rais wa awamu ya sita aliweka wazi kwa kuwaambia Simba anahitaji kuona wakimuita akiwakabidhi Kombe la Afrika jambo ambalo halijatimia mpaka anafikwa na umauti. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:”Rais wetu ameondoka ghafla na sisi Wanasimba tupo kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na tutashiriki kwa nguvu kubwa na ari ili kuenzi changamoto ambayo alituachia. " Tukiwa ni Wanasimba, wanasoka agizo lake linapaswa lituongoze ili hatimaye tufanikiwe kubeba taji la ubingwa wa Afrika,” . Kwa sasa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imetinga hatua ya makundi inaong...

FIFA YAMLILIA RAIS MAGUFULI

Image
    JUMUIYA ya soka kimataifa ‘FIFA’ limetuma salamu za rambirambi kwa shirikisho la soka nchini TFF kufuatia kifo cha Rais, Hayati, Dk.John Pombe Magufuli kilichoripotiwa kutokea siku ya Jumanne, 17 Machi 2021 kwenye Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi ya moyo.   Kwa niaba ya wajumbe wa jumuiya ya soka kimataifa, Rais wa jumuiya hiyo Gianni Infatino ameandika kuwa:- “Ilikuwa hisia ya huzuni kupata taarifa za kifo cha Rais Dk.John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.     “Tunapenda kuungana na wote wanaotoa salam za pole kutoka pande zote Duniani. Akiongoza toka mwaka 2015, kiongozi mwenye haiba ya juu, aliyetambulika kwa maono yake, uzalendo, matendo ya Utawala bora na kupiga vita rushwa na umasikini, Rais, Dk.John Pombe Magufuli hatosahaulika.   “Kwa niaba ya wajumbe wa jumuiya ya soka kimataifa, tunapenda kutoa pole kwa shrikisho la soka nchini Tanzania ‘TFF’, Serikali na watanzania kwenye kipindi hiki kigumu”....