MSUVA AITAMANI SIMBA ROBO FAINALI CAF

 

WINGA wa klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morroco, Saimon Msuva amesema kuwa anatamani kukutana  na klabu ya Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani anaamini itakuwa mechi nzuri sana katika msimu huu wa ligi hiyo.

Saimon Msuva katika msimu huu wa ligi hiyo akiwa na klabu ya Wydad Casablanca ya Morroco amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao miwili katika michezo minne aliyocheza mpaka sasa.

Akizungumzia michuano hiyo Msuva amesema: “Natamani kuona tunakutana na Simba katika hatua ya robo fainali kwani utakuwa mchezo mzuri sana katika ligi ya mabingwa msimu huu kwani itazikutanisha timu bora ambazo zote zinafanya vizuri kwa sasa.

Comments

Popular posts from this blog

UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI MAJANGA MATUPU AFCON

MASTAA SITA SIMBA WAIFUNIKA YANGA

KOCHA BIASHARA UNITED KUANZA KUONGEZA MAKALI YA WASHAMBULIAJI