Mambo 10 nilioyaona Coastal vs Yanga





1: What A Game✊ Tactically, Technically tumeshuhudia moja ya mechi bora kwenye VPL. Makocha wameshindana kwenye mbinu, wachezaji wakashindana kwenye ufundi. Fantastic Match🙌

2: Mgunda na Kaze walikuja na system  iliyofanana (4-2-4) lakini Coastal wakabadilika kwenye style of play na kuipoteza Yanga. Kivipi?

3: 4-2-4 ya Coastal iliswitch kwenye 4-3-3 kutokana na uwezo mkubwa wa Francis Mustafa katika kusoma mchezo👍 muda mwingi alidrop kucheza katikati ya mstari wa Mukoko na Fei.. Hii iliwapa Coastal power ya kuumiliki mchezo katikati ya kiwanja

4: System ya Kaze ilifelishwa na uchaguzi wake wa wachezaji. Kivipi? Fiston na Sarpong wote walicheza kama namba 9. Hakuna aliyejitolea kushuka chini. Farid na Kisinda wakawa wazito kurudi.. Timu ikatawanyika muda ambao ilitakiwa kuwa compact

5: Kwa system ile ya Kaze, Yacouba alistahili kuanza kwa Farid na Kaseke kuanza kwa Fiston au Sarpong. Kwa mtu aliyeifatilia Coastal Union hivi karibuni, ni kujitia kitanzi kuwapa 'space' kubwa wale vijana wao wakiwa na mpira

6: Pascal KITENGE🙌 What A Perfomance 👍 Alijitoa mwili na akili kuipambania nembo ya Coastal Union. Alikuwa mtawala, kiongozi na kikwazo cha mastraika wa Yanga. Nasubiri kuona muendelezo wa kiwango chake

7: Hamadi Majimengi.. What a Player🙌 Mchezaji mdogo anayeng'ara kwenye mechi kubwa✊ Mguu wake wa kushoto una maajabu ya kutosha. Ni kama 'pitch' ya Mkwakwani ilikua ikiathiri mikimbio yake

8: Nilipenda ustadi wa mabeki wa pembeni wa Coastal Union.. Kibailo na Hance Masoud🙌 Walikaba na kushambulia.. Ni somo kubwa ambalo wamelitoa kwa mabeki wa pembeni wa Yanga.. Angalau Shomari Kibwana.. Yassin alikuwa chini sana

9: Well done mwamuzi Raphael Ikambi👏 Mechi ngumu, presha kubwa lakini aliimudu kwa kiasi kikubwa. Kuna nyakati wachezaji walitaka kumtoa mchezoni lakini hakuyumba kwenye maamuzi yake

10: Abushehe anatakiwa kuketi chini na kutathimini ubora wake. Asilimia 90 ya pasi alizopiga zilipotea. Hili ni kwa Mwamnyeto pia. Iko kazi ya ziada anatakiwa kuifanya kuboresha utulivu wake anapopigwa presha

Nb: Wahuni wameitoa UnBeaten kwa Baikoko😀

Comments

Popular posts from this blog

MFARANSA WA SIMBA AFICHUA KINACHOWABEBA KIMATAIFA

FIFA YAMLILIA RAIS MAGUFULI

MSUVA AITAMANI SIMBA ROBO FAINALI CAF