KOCHA WA YANGA KAZE AKUBALI YAISHE MBELE YA COASTAL

 


KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa anaipongeza Coastal kwa ushindi walioupata dhidi ya klabu yake siku ya leo, huku pia akiwapongeza nyota wake kwa kupambana.

Yanga leo katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga imepoteza kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1.

Akizungumzia mchezo huo Kaze amesema: "Tulikuwa na mchezo mzuri dhidi ya wapinzani wetu na kufanikiwa kupata penalti mwanzoni, lakini kwa bahati mbaya tuliikosa.

"Lakini nawapongeza vijana wangu kwa kupambana, pamoja na wapinzani wetu kwa ushindi walioupata,"

Comments

Popular posts from this blog

MFARANSA WA SIMBA AFICHUA KINACHOWABEBA KIMATAIFA

BODI YA LIGI YATAJA SIKU YA MECHI ZA LIGI KUU BARA PAMOJA NA KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER HAJARIDHISHWA NA USHINDI WA MABAO 8-3