DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kikubwa ambacho kinawapa nguvu ya kuamini kwamba watapata matokeo mbele ya AS Vita ni pamoja na hali ya kujiamini na maandalizi mazuri. Kikosi cha Simba kinatarajiwa kumenyana na AS Vita kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa. Mfaransa huyo ameongeza kwamba kuchukulia siriazi na kujiamini katika mechi zao ndiyo kitu ambacho kimekuwa kikiwabeba na kuifanya timu hiyo kutopoteza mechi yoyote hadi sasa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba ni vinara wa Kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika watakuwa uwanjani kupambana na Vita katika mechi ambayo Simba wakitoa sare tu watajihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali, lakini Vita wanahitaji ushindi tu ili wafufue matumaini yao ya kutinga robo fainali. Gomes amesema kwamba kila mechi ambayo wamekuwa wakiicheza katika hatua hiyo wamekuwa wakiamini kwamba wanaweza kupata matokeo na hiyo imekuwa msaada mkubwa...
ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea Aprili 8 baada ya kutimiza siku 21 za maombolezo. Ligi ilisimama kwa muda kutokana na msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Joseph Magufuli ambapo zilitolewa siku 21 za maombolezo. Magufuli alitangulia mbele za haki Machi 17 jambo lilipolekea Serikali kutoa siku 21 za maombolezo ambazo bado zinaendelea kwa sasa. Kasongo amesema:- "Ukitazama ratiba yetu ile ya awali ambayo tuliitoa kwa vilabu ilikuwa inaonyesha kwamba tarehe 3-4 Machi, michezo ya Kombe la Shirikisho, tarehe 6-8 Machi tulikuwa tunarejea kwenye mechi za ligi. "Kutokana na msiba tafsiri yake ni kwamba ile michezo ya Shirikisho na ile ya ligi nayo inakuwa haipo kwa sababu tupo kwenye maombolezo ya siku 21. "Kumbuka kwamba siku 21 zinaisha tarehe 7 ambapo kulikuwa na mchezo wa ligi, tarehe 6 kulikuwa na mchezo wa ligi na tarehe 3-4 kulikuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho. ...
BONIPHACE Pawasa, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer) amesema kuwa hajaridhishwa na ushindi wa mabao 8-3 walioupata dhidi ya Burundi. Mchezo huo ambao uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa jana, Machi 30 ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwania tiketi ya kufuzu Afcon uliochezwa kwenye fukwe za Coco Beach, Dar. Pawasa amesema kuwa kwa namna ambavyo walijiandaa aliamini kwamba wangepata ushindi mkubwa zaidi ya huo ili kuongeza hali ya kujiamini kwa vijana wake. "Tulifanya maandalizi makubwa na mazuri jambo ambalo lilitupa matumaini kwamba tungepata ushindi mkubwa zaidi ya huu ambao tumeupata. "Kwa kuwa kuna makosa ambayo tumeyaona tutayafanyia kazi ili wakati ujao tuweze kupata matokeo mazuri zaidi ya hapa. "Ninawapongeza vijana kwa kazi ambayo wameifanya pamoja na sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa wakitupa nguvu sisi kufanya vizuri,". Mchezo mwingine wa marudio dhidi ya Burundi unatarajiwa kuchezwa Aprili 3,2021
Comments
Post a Comment