Posts

Showing posts from April, 2021

UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI MAJANGA MATUPU AFCON

Image
  UKANDA wa Afrika Mashariki mambo yamekuwa magumu kwenye mechi za kuwania kukata tiketi ya kufuzu kushiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika, (Afcon) kwa timu nyingi kuangukia pua. Sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 dhidi ya Cameroon inaifanya timu ya Taifa ya Rwanda nayo pia kuishia hatua ya makundi. Ni Cameroon na Cape Verde wamekata tiketi ya kushiriki Afcon nchini Cameroon baada ya kuwa nafasi mbili za juu ambapo mwenyeji Cameroon ana pointi 11 huku Cape Verde akiwa na pointi 10. Rwanda ipo nafasi ya 3 na pointi zao ni 6 huku nafasi ya nne ikiwa mikononi mwa Msumbiji wenye pointi 4 baada ya kucheza jumla ya mechi 6. Tanzania pia imeishia hatua ya makundi na pointi zake ni 7 katika kundi J ipo nafasi ya tatu ambapo ni Tunisia wenye pointi 16 na Equatorial Guinea wenye pointi 9 wamepenya mpaka Cameroon.  Burundi katika kundi E wapo nafasi ya tatu na pointi zao ni 5 huku Morocco yenye pointi 14 na Mauritania wenye pointi 9 wakitusua mpaka Cameroon.  Kenya katika kun...

USHINDI WA MABAO 14 WA TIMU YA TAIFA JAPAN WAWEKA REKODI

Image
  TIMU ya Taifa ya Japan, imeweka rekodi ya kupata ushindi mkubwa ambao haujawahi kutokea ndani ya dakika 90 katika harakati za kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Ushindi wa mabao 14-0 dhidi ya Mongolia walioupata Jumanne ya Machi 30 unawafanya wawe kwenye rekodi hiyo tamu huku wakiwa na nafasi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya 7. Walikuwa hawajacheza tangu Novemba 2019 kutokana na janga la Virusi vya Corona.  Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Fuku-Ari dakika 90 wapinzani wa Japan walikamilisha bila kupiga shuti hata moja lililolenga lango huku Japan ikipiga jumla ya mashuti 25 ambayo yalilenga lango la wapinzani hao  Matokeo hayo yanaifanya Japan kuwa nafasi ya kwanza katika kundi F na pointi zao ni 15 baada ya kucheza mechi 5 huku Mongolia ikiwa nafasi ya tano na pointi zao ni 3 baada ya kucheza mechi 7. Mshambuliaji wa Southampton ambaye yupo huko kwa mkopo akitokea Klabu ya Liverpool, Takumi Minamino alifungulia mvua ya mabao dk 13 kwenye mchezo huo. Kazi ikaen...

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER HAJARIDHISHWA NA USHINDI WA MABAO 8-3

Image
  BONIPHACE Pawasa, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer) amesema kuwa hajaridhishwa na ushindi wa mabao 8-3 walioupata dhidi ya Burundi. Mchezo huo ambao uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa jana, Machi 30  ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwania tiketi ya kufuzu Afcon uliochezwa kwenye fukwe za Coco Beach, Dar. Pawasa amesema kuwa kwa namna ambavyo walijiandaa aliamini kwamba wangepata ushindi mkubwa zaidi ya huo ili kuongeza hali ya kujiamini kwa vijana wake. "Tulifanya maandalizi makubwa na mazuri jambo ambalo lilitupa matumaini kwamba tungepata ushindi mkubwa zaidi ya huu ambao tumeupata. "Kwa kuwa kuna makosa ambayo tumeyaona tutayafanyia kazi ili wakati ujao tuweze kupata matokeo mazuri zaidi ya hapa. "Ninawapongeza vijana kwa kazi ambayo wameifanya pamoja na sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa wakitupa nguvu sisi kufanya vizuri,". Mchezo mwingine wa marudio dhidi ya Burundi unatarajiwa kuchezwa Aprili 3,2021