Posts

UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI MAJANGA MATUPU AFCON

Image
  UKANDA wa Afrika Mashariki mambo yamekuwa magumu kwenye mechi za kuwania kukata tiketi ya kufuzu kushiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika, (Afcon) kwa timu nyingi kuangukia pua. Sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 dhidi ya Cameroon inaifanya timu ya Taifa ya Rwanda nayo pia kuishia hatua ya makundi. Ni Cameroon na Cape Verde wamekata tiketi ya kushiriki Afcon nchini Cameroon baada ya kuwa nafasi mbili za juu ambapo mwenyeji Cameroon ana pointi 11 huku Cape Verde akiwa na pointi 10. Rwanda ipo nafasi ya 3 na pointi zao ni 6 huku nafasi ya nne ikiwa mikononi mwa Msumbiji wenye pointi 4 baada ya kucheza jumla ya mechi 6. Tanzania pia imeishia hatua ya makundi na pointi zake ni 7 katika kundi J ipo nafasi ya tatu ambapo ni Tunisia wenye pointi 16 na Equatorial Guinea wenye pointi 9 wamepenya mpaka Cameroon.  Burundi katika kundi E wapo nafasi ya tatu na pointi zao ni 5 huku Morocco yenye pointi 14 na Mauritania wenye pointi 9 wakitusua mpaka Cameroon.  Kenya katika kun...

USHINDI WA MABAO 14 WA TIMU YA TAIFA JAPAN WAWEKA REKODI

Image
  TIMU ya Taifa ya Japan, imeweka rekodi ya kupata ushindi mkubwa ambao haujawahi kutokea ndani ya dakika 90 katika harakati za kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Ushindi wa mabao 14-0 dhidi ya Mongolia walioupata Jumanne ya Machi 30 unawafanya wawe kwenye rekodi hiyo tamu huku wakiwa na nafasi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya 7. Walikuwa hawajacheza tangu Novemba 2019 kutokana na janga la Virusi vya Corona.  Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Fuku-Ari dakika 90 wapinzani wa Japan walikamilisha bila kupiga shuti hata moja lililolenga lango huku Japan ikipiga jumla ya mashuti 25 ambayo yalilenga lango la wapinzani hao  Matokeo hayo yanaifanya Japan kuwa nafasi ya kwanza katika kundi F na pointi zao ni 15 baada ya kucheza mechi 5 huku Mongolia ikiwa nafasi ya tano na pointi zao ni 3 baada ya kucheza mechi 7. Mshambuliaji wa Southampton ambaye yupo huko kwa mkopo akitokea Klabu ya Liverpool, Takumi Minamino alifungulia mvua ya mabao dk 13 kwenye mchezo huo. Kazi ikaen...

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER HAJARIDHISHWA NA USHINDI WA MABAO 8-3

Image
  BONIPHACE Pawasa, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer) amesema kuwa hajaridhishwa na ushindi wa mabao 8-3 walioupata dhidi ya Burundi. Mchezo huo ambao uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa jana, Machi 30  ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwania tiketi ya kufuzu Afcon uliochezwa kwenye fukwe za Coco Beach, Dar. Pawasa amesema kuwa kwa namna ambavyo walijiandaa aliamini kwamba wangepata ushindi mkubwa zaidi ya huo ili kuongeza hali ya kujiamini kwa vijana wake. "Tulifanya maandalizi makubwa na mazuri jambo ambalo lilitupa matumaini kwamba tungepata ushindi mkubwa zaidi ya huu ambao tumeupata. "Kwa kuwa kuna makosa ambayo tumeyaona tutayafanyia kazi ili wakati ujao tuweze kupata matokeo mazuri zaidi ya hapa. "Ninawapongeza vijana kwa kazi ambayo wameifanya pamoja na sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa wakitupa nguvu sisi kufanya vizuri,". Mchezo mwingine wa marudio dhidi ya Burundi unatarajiwa kuchezwa Aprili 3,2021

EYMAEL: KUIFUNGA SIMBA MBELE YA JPM NI KUMBUKUMBU KWANGU NA WACHEZAJI

Image
   LUC Eymael, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2019/20 amesema kuwa moja ya kitu ambacho anakikumbuka muda wote ni ushindi wake mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 8,2020 na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Simba. Bao pekee ambalo alilishuhudia pia aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli lilipachikwa kimiani na Bernard Morrison na kuwafanya Simba wayeyushe pointi tatu. Kwa sasa baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki Machi 17,2021 Samia Suluhu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa katiba ambapo awali alikuwa ni makamu wa JPM. Leo Machi 30, Samia amemchagua Philip Mpango awe Makamu wa Rais wa Tanzania ambapo jina lake limepitishwa na Wabunge kwa asilimia 100. Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael ambaye kwa sasa yupo Ubelgiji amesema kuwa anakumbuka mchezo huo kwa namna ambavyo Magufuli aliweza kuhudhuria na timu yake ilishinda jambo ambalo hal...

AS VITA WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA WAANZA KUMWAGA SABABU KIBAO

Image
    ZIKIWA zimesalia siku chache kufikia siku ya mtanange kati ya Simba na AS Vita, Kocha Mkuu wa AS Vita kutoka nchini DR Congo, Florent Ibenge ameweka wazi kuwa ratiba yake ya sasa si rafiki kwa klabu hiyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba. Ibenge ukiachana na kuwa kocha wa AS Vita, pia ni kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Congo ambapo Jumatatu aliongoza taifa la Congo katika mchezo wao wa mwisho wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika dhidi ya Gambia. Kwenye mchezo huo Ibenge alishuhudia kikosi chake kikishinda bao 1-0 ila kilikwama kufuzu Afcon nchini Cameroon kwa kuwa kipo nafasi ya tatu.   Ibenge amesema kuwa ratiba ya mechi za timu za taifa na michuano ya Ligi ya Mabingwa imebana sana kiasi cha kukosa siku za kutosha kwake kukiandaa kikosi cha AS Vita kuelekea mchezo wao unaofuata wa michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Simba.     “Ratiba si rafiki kwetu, nadhani hii ni kwa klabu nyingi zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa, ukiangalia mechi za timu za...

KOCHA BIASHARA UNITED KUANZA KUONGEZA MAKALI YA WASHAMBULIAJI

Image
   KOCHA Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Francis Baraza amesema kuwa kazi ya kwanza atakayoanza nayo kwa sasa ni kushughulika na safu ya ushambuliaji ili irejeshe makali yake. Baraza amechukua mikoba ya Mecky Maxime ambaye alifutwa kazi kutokana na mwendo mbovu wa timu yake na mchezo wa mwisho kukaa benchi ilikuwa mbele ya Azam FC ambapo ubao wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 1-2 Azam FC. Kwa sasa Maxime yupo huru ambapo amekuwa akitajwa kuibukia Biashara United kuchukua mikoba ya Baraza. Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa amewatazama washambuliaji wake walivyo na ameona ni lazima aanze nao ili kuongeza kasi kwenye ushambuliaji. "Ili timu ipate ushindi ni lazima ifunge na ufungaji unaanzia kwa washambuliaji pamoja na viungo ambao kazi yao ni kutengeneza nafasi za kufunga kwa washambuliaji. "Kikubwa ambacho nina amini kwamba kinawezekana ni kupata matokeo katika mechi zetu hivyo mashabiki watupe sapoti bila kuwa na mashaka nasi," . Kagera Sugar kwenye msimamo ipo...

BODI YA LIGI YATAJA SIKU YA MECHI ZA LIGI KUU BARA PAMOJA NA KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA

Image
  ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea Aprili 8 baada ya kutimiza siku 21 za maombolezo. Ligi ilisimama kwa muda kutokana na msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Joseph Magufuli ambapo zilitolewa siku 21 za maombolezo. Magufuli alitangulia mbele za haki Machi 17 jambo lilipolekea Serikali kutoa siku 21 za maombolezo ambazo bado zinaendelea kwa sasa. Kasongo amesema:- "Ukitazama ratiba yetu ile ya awali ambayo tuliitoa kwa vilabu ilikuwa inaonyesha kwamba tarehe 3-4 Machi, michezo ya Kombe la Shirikisho, tarehe 6-8 Machi tulikuwa tunarejea kwenye mechi za ligi. "Kutokana na msiba tafsiri yake ni kwamba ile michezo ya Shirikisho na ile ya ligi nayo inakuwa haipo kwa sababu tupo kwenye maombolezo ya siku 21. "Kumbuka kwamba siku 21 zinaisha tarehe 7 ambapo kulikuwa na mchezo wa ligi, tarehe 6 kulikuwa na mchezo wa ligi na tarehe 3-4 kulikuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho. ...